Aal-i-Imraan 3:104
آل عمرانوَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى ٱلْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِٱلْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ ۚ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ
Na uwepo umma miongoni mwenu wanaoilingania heri, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu. Na hao ndio waliofaulu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa. [104]
[104] Hakika njia ya kuungana kuliko kamilika juu ya Haki katika kivuli cha Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kivuli cha Mtume wake, ni kuwa muwe nyinyi Umma unao lingania (unao itia) watu waje wafuate mwendo utao waletea maslaha ya Dini na dunia, uamrishe ut'iifu kwa Mwenyezi Mungu, ukataze maasia. Na hapo ndipo mtakuwa mlio fuzu, kufuzu kulio kamilika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kiweko miongoni mwenu, enyi Waumini, kikundi kitakacholingania katika kheri, kiamrishe mema, nayo ni yale yanayojulikana uzuri wake kisheria na kiakili, na kikataze maovu, nayo ni yale yanayojulikana uovu wake kisheria na kiakili. Na hao ndio watakaofaulu kupata Pepo zenye neema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net