Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 105

Aal-i-Imraan 3:105

آل عمران

وَلَا تَكُونُوا۟ كَٱلَّذِينَ تَفَرَّقُوا۟ وَٱخْتَلَفُوا۟ مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلْبَيِّنَـٰتُ ۚ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Maana

Wala msiwe kama wale waliotengana na wakahitilafiana baada ya kufikiwa na hoja zilizo wazi. Na hao ndio wana adhabu kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala msiwe kama wale walio farikiana na kukhitalifiana baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi. Na hao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa. [105]

[105] Wala msiwe kwa kupuuza kwenu kuamrisha mema na kukataza maovu--mambo ambayo ndiyo yanayo kukusanyeni katika kheri na Dini ya Haki--kama wale walio puuza kuamrisha mema na kukataza maovu,wakagawika mapande mbali mbali, wakakhitalifiana katika Dini yao baada ya kuwafikilia hoja zilizo wazi, zenye kubainisha Haki. Na hao walio farikiana wakakhitalifiana, watapata adhabu kuu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wala msiwe, enyi Waumini, kama waliopewa vitabu, ambao ulizuka uadui kati yao na kuchukiana, wakatengana makundi na vyama mbalimbali na wakatafautiana kwenye misingi ya dini yao baada ya haki kuwa wazi kwao. Na hao wanastahili adhabu kubwa iumizayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net