Aal-i-Imraan 3:92
آل عمرانلَن تَنَالُوا۟ ٱلْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا۟ مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا۟ مِن شَىْءٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٌ
Kamwe hamtaufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachokitoa, basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua vyema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
KABISA HAMTAFIKIA wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda. Na kitu chochote mnacho kitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua. [92]
[92] Enyi Waumini! Hamtoipata kheri kaamili mnayo itaka na itakayo mridhisha Mwenyezi Mungu ila mkitoa katika vitu mnavyo vipenda na mkatoa katika Sabili Llahi, Njia ya Mwenyezi Mungu, kwa namna mbali mbali. Na chochote mnacho kitoa, kidogo na kikubwa, kilio bora au chenginecho, Mwenyezi Mungu anakijua. Kwani Yeye ni Mwenye Kujua, hapana kitu kilioko mbinguni au duniani kinacho fichikana naye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hamuwezi kupata Pepo ng’o! mpaka mtoe sadaka katika vile vitu mnavyovipenda. Na chochote mnachokitoa sadaka, kiwe ni kichache au ni kingi, basi Allah Mtukufu Anakijua mno na Atamlipa kila mtoaji malipo yanayolingana na kitendo chake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net