Aal-i-Imraan 3:91
آل عمرانإِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَمَاتُوا۟ وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ ٱلْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ ٱفْتَدَىٰ بِهِۦٓ ۗ أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّـٰصِرِينَ
Hakika, wale waliokufuru, na wakafa hali ya kuwa ni makafiri, haitakubaliwa kutoka kwa yeyote wao fidia ya dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wangeliitoa. Hao wana adhabu chungu, wala hawatakuwa na wowote wa kuwanusuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wale walio kufuru, na wakafa hali ni makafiri haitakubaliwa kutoka kwa yeyote wao fidia ya dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wangeli itoa. Hao watapata adhabu chungu, wala hawatakuwa na wa kuwanusuru. [91]
[91] Wale wanao ipinga Haki wala hawaifuati, na wanaendelea na uwovu wao mpaka wakafa nao ni wapinzani tu, basi yeyote miongoni mwao hawezi kujitolea fidia ya kujiepusha na adhabu ya Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la, hata ikawa anacho kitoa kuwa fidia ni dhahabu ya kujaza dunia nzima kama angeweza. Na adhabu yao ina uchungu mkali.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale waliokanusha unabii wa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na wakafa juu ya kumkufuru Allah Mtukufu na Mtume Wake, haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao, Siku ya Kiyama, dhahabu iliyojaa ardhi iwe ni fidia ya nafsi yake kutokana na adhabu ya Allah Mtukufu, lau atajikomboa nayo kikweli. Wao wana adhabu yenye kuumiza; na hawana yoyote wa kuwaokoa na adhabu ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net