Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 90

Aal-i-Imraan 3:90

آل عمران

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بَعْدَ إِيمَـٰنِهِمْ ثُمَّ ٱزْدَادُوا۟ كُفْرًا لَّن تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلضَّآلُّونَ

Maana

Hakika, wale waliokufuru baada ya kuamini kwao, kisha wakazidi kukufuru, haitakubaliwa toba yao, na hao ndio waliopotea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale walio kufuru baada ya kuamini kwao, kisha wakazidi kukufuru, toba yao haitakubaliwa, na hao ndio walio potea. [90]

[90] Kukubaliwa toba na kupata rehema ya maghfira kunashurutishwa mtu adumu juu ya Imani. Wanao ipinga Haki baada ya ut'iifu na kusadiki, na wakazidisha upinzani na ufisadi na kuwaudhi Waumini, Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la hatokubali toba yao. Haiwezi kuwa toba yao hiyo ni kweli na safi na hali wanaendelea na vitendo vyao, wapo mbali na Haki na wanaigeuzia nyuso zao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale waliokufuru baada ya kuwa wao wameamini na wakaendelea kwenye ukafiri mpaka kufa, haitakubaliwa toba kutoka kwao mauti yakiwasimamia. Na wao ndio waliopotea njia wakakosa kuifikia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net