Aal-i-Imraan 3:89
آل عمرانإِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُوا۟ مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengenea. Basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Isipo kuwa wale walio tubu baada ya hayo na wakatengenea; kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. [89]
[89] Lakini wale ambao wamejing'oa na madhambi yao, wakaingia kati ya watu wema, wakayaondoa waliyo yaharibu, basi hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu atawafutia madhambi yao, kwani maghfira na rehema ni miongoni mwa sifa za dhati yake Tukufu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Isipokuwa waliorudi kwa Mola wao kwa kutubia kidhati baada ya ukafiri wao na udhalimu wao na wakayatengeneza, kwa toba yao, waliyoyaharibu. Allah Mtukufu Ataikubali hiyo toba, kwani Yeye ni Mwingi wa kusamehe madhambi ya waja wake, ni Mwenye huruma kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net