Aal-i-Imraan 3:69
آل عمرانوَدَّت طَّآئِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ لَوْ يُضِلُّونَكُمْ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ
Kilipenda kikundi katika Watu wa Kitabu lau kuwa wangekupotezeni. Lakini hawapotezi isipokuwa nafsi zao, nao wenyewe hawatambui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kipo kikundi katika Watu wa Kitabu wanao penda kukupotezeni; lakini hawapotezi ila nafsi zao, nao wenyewe hawatambui. [69]
[69] Kipo kikundi katika Watu wa Kitabu wanao tamani kuwapotoa Waumini na kuwafitini waache Dini yao, kwa kuwatilia mikorogo ya kudhoofisha itikadi. Lakini katika kazi yao hii hawatampotoa mtu ila nafsi zao wenyewe kwa kuendelea katika upotovu, ambao utakuja kuwagubika wao wenyewe tu, na wala hawajui kuwa matokeo ya juhudi yao ovu yatawapata wenyewe, wala hayatawadhuru Waumini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Lilitamani kundi la Mayahudi na Manaswara lau wangaliwapoteza nyinyi, enyi Waislamu, wakawatoa kwenye Uislamu. Wao hawampotezi yoyote isipokuwa nafsi zao na wafuasi wao; na wao hawalielewi hilo wala hawalijui.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net