Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 68

Aal-i-Imraan 3:68

آل عمران

إِنَّ أَوْلَى ٱلنَّاسِ بِإِبْرَٰهِيمَ لَلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ وَهَـٰذَا ٱلنَّبِىُّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ۗ وَٱللَّهُ وَلِىُّ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Hakika, watu wanaomstahiki zaidi Ibrahim ni wale waliomfuata yeye, na Nabii huyu na wale walioamini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Kipenzi Mlinzi wa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watu wanao mkaribia zaidi Ibrahim ni wale walio mfuata yeye na Nabii huyu na walio amini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa Waumini. [68]

[68] Hakika wenye haki kabisa kunasibiana na Ibrahim na Dini yake ni wale walio mwitikia wito wake na wakaongoka kufuata uwongofu wake katika zama zake, na vile vile Muhammad s.a.w. na walioamini pamoja naye. Kwani hao ni watu wa Tawhidi safi ya kweli, kumwamini Mwenyezi Mungu mmoja bila ya walakini. Hiyo ndiyo Dini ya Ibrahim. Mwenyezi Mungu anawapenda Waumini, na Yeye atawanusuru, kwani wao ni vipenzi vyake, na atawalipa kwa mema na ziada.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wenye haki zaidi na Ibrãhîm na wanaohusika naye zaidi ni wale waliomuamini, wakausadiki utume wake na wakaifuata dini yake na huyu Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na waliomuamini yeye.Na Allah Mtukufu ni Msaidizi wa wenye kumuamini yeye na kufuata Sheria Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net