Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 67

Aal-i-Imraan 3:67

آل عمران

مَا كَانَ إِبْرَٰهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ

Maana

Ibrahim hakuwa Myahudi wala Mkristo. Lakini alikuwa mnyoofu, Muislamu, na wala hakuwa katika washirikina.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina. [67]

[67] Hakika Ibrahim a.s. hakufuata dini ya Kiyahudi wala dini ya Kikristo, lakini ameachana na dini zote za upotovu na akashika Dini ya Haki, ya Uislamu, yaani kumwelekea Mwenyezi Mungu, na kumtakasia Yeye kwa ut'iifu, na wala hakuwa miongoni wa hao wanao mshirikisha Mwenyezi Mungu katika kuabudu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ibrãhîm hakuwa ni Myahudi wala Mnaswara, kwa kuwa Uyahudi haukuwa, wala Unaswara, isipokuwa baada yake. Lakini alikuwa mfuasi na mtiifu wa amri ya Allah Mtukufu, aliyejisalimisha Kwake, na hakuwa ni miongoni mwa washirikina.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net