Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 66

Aal-i-Imraan 3:66

آل عمران

هَـٰٓأَنتُمْ هَـٰٓؤُلَآءِ حَـٰجَجْتُمْ فِيمَا لَكُم بِهِۦ عِلْمٌ فَلِمَ تُحَآجُّونَ فِيمَا لَيْسَ لَكُم بِهِۦ عِلْمٌ ۚ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

Maana

Angalieni! Nyinyi mlibishana katika yale mliyoyajua. Mbona sasa mnabishana katika yale msiyoyajua? Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye, na nyinyi hamjui.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Angalieni! Nyinyi mlibishana katika yale mliyo yajua. Mbona sasa mnabishana katika yale msiyo yajua? Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye, na nyinyi hamjui. [66]

[66] Watu nyinyi mlikuwa mkijadili mambo yalio wakhusu Musa na Isa mnayo yajua kama mnavyo dai wenyewe. Imekuwaje basi hivi sasa kudai kuwa Ibrahim alikuwa Yahudi au Mkristo - jambo ambalo nyinyi hamlijui! Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kujua hakika ya hayo mnayo gombania, na nyinyi hamjui kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ndio nyinyi mliomjadili Mtume wa Allah Mtukufu, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, juu ya mambo ya dini yenu ambayo muna ujuzi nayo, katika yale yaliyomo ndani ya vitabu vyenu mnayoitakidi usahihi wake. Lakini ni kwa nini nyinyi mnayajadili mambo ya Ibrãhîm ambayo hamuna ujuzi nayo? Na Allah Mtukufu Anayajua mambo pamoja na kuwa yamefichika, na nyinyi hamjui.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net