Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 65

Aal-i-Imraan 3:65

آل عمران

يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ لِمَ تُحَآجُّونَ فِىٓ إِبْرَٰهِيمَ وَمَآ أُنزِلَتِ ٱلتَّوْرَىٰةُ وَٱلْإِنجِيلُ إِلَّا مِنۢ بَعْدِهِۦٓ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ

Maana

Enyi Watu wa Kitabu! Mbona mnabishana juu ya Ibrahim, na hali Taurati na Injili havikuteremshwa isipokuwa baada yake? Kwani hamtumii akili?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi Watu wa Kitabu! Mbona mnabishana juu ya Ibrahim, na hali Taurati na Injili hazikuteremshwa ila baada yake? Basi hamzingatii? [65]

[65] Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnazozana na kujadiliana kwa mambo ya Ibrahim, kila mmoja wenu akidai kuwa yeye ndiye anaishika dini yake, na ilhali Ibrahim alikuwako kabla ya Taurati na Injili akifuata sharia mbali. Hizo Taurati na Injili hazikuja ila baadae. Basi atakuwaje yeye afuate sharia za vitabu hivyo? Hamna akili ya kutambua jambo hili lilio wazi?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu wa vitabu vilivyoteremshwa, miongoni Mwa Mayahudi na Wanaswara, vipi kila mmoja kati yenu anabisha kwamba Ibrãhîm, amani imshukie, alikuwa kwenye mila yake. Ilhali Taurati na Injili hazikuteremshwa ila baada yake? Kwani hamufahamu upotofu wa maneno yenu kwamba Ibrãhîm alikuwa Myahudi au Mnaswara, na hali mnajua kuwa Uyahudi na Unaswara ulizuka baada ya kufa kwake kwa muda?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net