Aal-i-Imraan 3:64
آل عمرانقُلْ يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ تَعَالَوْا۟ إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَآءٍۭ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا ٱللَّهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِۦ شَيْـًٔا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ ٱللَّهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَقُولُوا۟ ٱشْهَدُوا۟ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ
Sema: 'Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lililo sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote. Wala tusifanyane waungu sisi kwa sisi badala ya Mwenyezi Mungu.' Na wakigeuka, basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi kwa hakika ni Waislamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni Waislamu. [64]
[64] Sema, ewe Nabii! Enyi Watu wa Kitabu! (Biblia, yaani Mayahudi na Wakristo) njooni kwenye neno moja la uadilifu lenye kutukusanya sote na tunalo litaja, nalo ni kuwa hatumuabudu ila Mwenyezi Mungu tu, wala tusimwekee washirika katika ibada. Na wala tusiwe tunawat'ii baadhi yetu tukiwafuata katika kuhalalisha na kuharimisha, tukaachilia mbali hukumu ya Mwenyezi Mungu katika mambo ya halali na haramu. Wakiukataa wito huu wa haki waambie: Shuhudieni kuwa sisi ni Waislamu, yaani tunafuata hukumu za Mwenyezi Mungu, na Yeye tu tumemsafia Dini, wala hatumwombi mwengineyo. (Taurati:Kutoka 20.3:Usiwe na miungu mingine ila Mimi. Injili ya Marko 12.29 : Yesu akamjibu, [amri] Ya kwanza ndiyo hii, Sikia Israel, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja.)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia Watu wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, «Njooni kwenye neno la uadilifu na haki tushikamane nalo sote. Nalo ni sisi kuielekeza ibada yetu kwa Allah Mtukufu Peke Yake. Na tusimfanye yoyote kuwa ni mshirika pamoja na Yeye, awe ni sanamu au msalaba au Shetani au kinginecho. Na wala wasiwadhalilikie baadhi yetu watu wengine kwa kuwatii badala ya Allah Mtukufu.» Basi wakiukataa mwito huu mzuri, waambieni wao, enyi Waumini, «Kuweni ni mashahidi kwetu kuwa sisi tumejisalimisha kwa Mola wetu na tumenyosha shingo zetu Kwake kwa kukubali kuwa ni waja Wake na kwa kumtakasa.» Na mwito huu kwenye neno la sawa, kama unavyoelekezwa kwa Mayahudi na Wanaswara, unaelekezwa pia kwa wenye mwenendo kama wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net