Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 63

Aal-i-Imraan 3:63

آل عمران

فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌۢ بِٱلْمُفْسِدِينَ

Maana

Na wakigeuka, basi Mwenyezi Mungu anawajua mno waharibifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kama wakigeuka basi Mwenyezi Mungu anawajua waharibifu. [63]

[63] Wakiikataa Haki baada ya kwisha wadhihirikia, na wasiache upotovu wao, basi hao ndio waharibifu. Na Mwenyezi Mungu anawajua.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wakikataa kukuamini na kukufuata, basi wao ndio waharibifu. Na Allah Mtukufu Anawajua na Atawalipa kwa hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net