Aal-i-Imraan 3:62
آل عمرانإِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ ٱلْقَصَصُ ٱلْحَقُّ ۚ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا ٱللَّهُ ۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ
Hakika, haya ndiyo maelezo ya kweli. Na hakuna mungu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika haya ndiyo maelezo ya kweli. Na hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu tu, na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hikima. [62]
[62] Hiyo ndiyo kweli isiyo na shaka yoyote. Kwani hapanapo mungu ila Mwenyezi Mungu aliye umba kila kitu, na Yeye ni pekee katika utukufu wa Ufalme wake na hikima katika uumbaji wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika hili nililokuhadithia, ewe Mtume, kuhusu mambo ya ‛Ĩsã ndio habari ya kweli isiyo na shaka. Na hakuna muabudiwa anayestahiki ibada isipokuwa ni Allah Mtukufu Peke Yake. Na hakika Allah Mtukufu Ndiye Mshindi katika ufalme Wake, Ndiye Mwenye hekima katika upelekaji mambo Wake na vitendo Vyake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net