Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 61

Aal-i-Imraan 3:61

آل عمران

فَمَنْ حَآجَّكَ فِيهِ مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلْعِلْمِ فَقُلْ تَعَالَوْا۟ نَدْعُ أَبْنَآءَنَا وَأَبْنَآءَكُمْ وَنِسَآءَنَا وَنِسَآءَكُمْ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمْ ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَل لَّعْنَتَ ٱللَّهِ عَلَى ٱلْكَـٰذِبِينَ

Maana

Basi mwenye kukuhoji katika haya baada ya yale yaliyokufikia katika elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wake zetu na wake zenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikilia ilimu hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wake zetu na wake zenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo. [61]

[61] Basi wenye kujadiliana nawe, ewe Nabii, katika shani ya Isa baada ya kukujia wewe khabari iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu na ambayo haina ubabaifu ndani yake, basi waambie kauli itakayo dhihirisha ujuzi wako wa yakini na upotovu wao wa uwongo: Njooni! Kila mmoja wetu na wenu awaite watoto wake, na wakeze na wenyewe nafsi zao. Kisha tumnyenyekee Mwenyezi Mungu kumtaka ateremshe ghadhabu yake na nakama yake juu ya aliye mwongo katika hili jambo la Isa kuzaliwa bila ya baba na kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu wala si Mwana wa Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi yoyote mwenye kujadiliana nawe, ewe Mtume, kuhusu Al-Masîḥ ‛Ĩsã mwana wa Maryam, baada ya ujuzi uliokufikia juu ya ‛Ĩsã, amani imshukie, waambie, «Njooni tuwahudhurishe watoto wetu wa kiume na watoto wenu wa kiume, wanawake wetu na wanawake wenu na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuelekee kwa Allah Mtukufu kwa kumuomba Ayashukishe mateso Yake na laana Yake juu ya warongo katika maneno yao, wenye kuendelea katika upotofu wao».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net