Aal-i-Imraan 3:60
آل عمرانٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُن مِّنَ ٱلْمُمْتَرِينَ
Hii ni haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanaofanya shaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanao fanya shaka. [60]
[60] Bayana hii katika kuumbwa Isa ndiyo ukweli wenyewe ambao unabainisha hakika yaliyo tokea katika khabari za Mola Mlezi wa viumbe vyote. Basi wewe dumu katika yakini yako wala usiwe katika wenye kutia shaka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Haki isiyo na shaka kuhusu mambo ya ‛Ĩsã ni ile iliyokujia, ewe Mtume, kutoka kwa Mola wako. Endelea kwenye yakini yako na juu ya msimamo ulionao wa kuacha uzushi. Na usiwe ni miongoni mwa wenye shaka. Katika haya pana kumtia moyo Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na kumtuliza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net