Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 59

Aal-i-Imraan 3:59

آل عمران

إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ ٱللَّهِ كَمَثَلِ ءَادَمَ ۖ خَلَقَهُۥ مِن تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

Maana

Hakika, mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam. Alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: 'Kuwa!' Basi akawa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa. [59]

[59] Baadhi ya watu wamepotea katika kadhiya ya Isa, wakadai ati kuwa yeye ni Mwana wa Mwenyezi Mungu kwa kuwa kazaliwa bila ya baba. Mwenyezi Mungu anawaambia: Hakika shani ya Isa katika kuumbwa kwake bila ya baba ni kama shani ya Adam alivyo umbwa kwa udongo bila ya baba wala mama. Mwenyezi Mungu alimfanya na akataka awe, akawa mtu sawasawa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika mfano wa Allah Mtukufu kumuumba ‛Ĩsã, bila ya baba, ni kama mfano wa Allah Mtukufu kumuumba Ãdam, bila ya baba wala mama. Allah Mtukufu Alimuumba kutokana na mchanga wa ardhi kisha Akamwabia, «kuwa kiumbe», akawa. Basi madai ya uungu wa ‛Ĩsã kwa kuwa aliumbwa bila ya baba, ni madai ya urongo. Ãdam, amani imshukie, aliumbwa bila ya baba wala mama, na wote wamekubaliana kwamba yeye ni mja miongoni mwa waja wa Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net