Aal-i-Imraan 3:58
آل عمرانذَٰلِكَ نَتْلُوهُ عَلَيْكَ مِنَ ٱلْـَٔايَـٰتِ وَٱلذِّكْرِ ٱلْحَكِيمِ
Haya tunayokusomea ni katika Aya na ukumbusho wenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Haya tunayo kusomea ni katika Aya na Ukumbusho wenye hikima. [58]
[58] Hayo tuliyo kusimulia ni miongoni ya hoja zenye kuonyesha ukweli wa ujumbe wako, nayo ni katika Qur'ani Tukufu yenye kukumbusha, na yenye kukusanya ilimu ya manufaa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hayo tuliyokusimulia kuhusu habari ya ‛Ĩsã ni miongoni mwa dalili zilizo wazi za usahihi wa utume wako na usahihi wa Qur’ani yenye hekima inayopambanua baina ya haki na batili; haina shaka wala ubishi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net