Aal-i-Imraan 3:57
آل عمرانوَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na ama wale walioamini na wakatenda mema, basi Mwenyezi Mungu atawalipa ujira wao kamili. Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ama wale walio amini na wakatenda mema basi Mwenyezi Mungu atawalipa ujira wao kaamili. Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhaalimu. [57]
[57] Na ama walio ongoka kwa uwongofu wa Mwenyezi Mungu, wakatenda vitendo vya kufuata mwendo wa kheri, Mwenyezi Mungu atawapa malipo ya kutosha kwa hizo a'mali zao. Na ndiyo shani yake Mwenyezi Mungu kuwa hawalipi thawabu zake wale wanao pindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu wakafanya jeuri ya kutoitikia wito wake na kumtendea wema. Wala hawanyanyulii cheo chao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ama wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mitume Wake na wakafanya matendo mema, Allah Mtukufu Atawapa thawabu za matendo yao zikiwa kamili zisizopunguzwa. Na Allah Mtukufu Hawapendi wenye kujidhulumu kwa ushirikina na ukafiri.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net