Aal-i-Imraan 3:56
آل عمرانفَأَمَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَأُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّـٰصِرِينَ
Ama wale waliokufuru, basi nitawaadhibu adhabu kali katika dunia na Akhera, na wala hawatapata wowote wa kuwanusuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ama wale walio kufuru, nitawaadhibu adhabu kali katika dunia na Akhera, wala hawatapata wa kuwanusuru. [56]
[56] Ama wale wanao kataa kwa ukafiri nitawaonjesha adhabu ya hizaya na mateso kwa kuwasalitisha mataifa mengine juu yao katika dunia, na hakika adhabu ya Akhera ni kali zaidi na ina hizaya zaidi. Na wala hawana wa kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ama wale waliomkanusha al- Masîḥ miongoni mwa Mayahudi, au wakamzidishia sifa miongoni mwa Wanaswara, nitawaadhibu adhabu kali katika ulimwengu: kwa kuuawa, kunyang’anywa mali na kuondolewa ufalme, na katika Akhera kwa Moto; na hawatakuwa na msaidizi mwenye kuwanusuru na kuwaepushia adhabu ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net