Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 55

Aal-i-Imraan 3:55

آل عمران

إِذْ قَالَ ٱللَّهُ يَـٰعِيسَىٰٓ إِنِّى مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَىَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَجَاعِلُ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوكَ فَوْقَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۖ ثُمَّ إِلَىَّ مَرْجِعُكُمْ فَأَحْكُمُ بَيْنَكُمْ فِيمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ

Maana

Pale Mwenyezi Mungu aliposema: Ewe Isa, hakika Mimi nitakuchukua (bila kukufisha), na nitakunyanyua hadi kwangu, na nitakutakasa kutokana na wale waliokufuru, na nitawaweka wale waliokufuata juu ya wale waliokufuru, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha kwangu ndiko marejeo yenu, na nihukumu kati yenu katika yale mliyokuwa mkihitilafiana.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka wale walio kufuata juu ya wale walio kufuru, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu yatakuwa kwangu, nikuhukumuni katika yale mliyo kuwa mkikhitalifiana. [55]

[55] Taja ewe Nabii, pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa Mimi nitakutimizia ajali yako,(yaani nitakufisha kifo cha kawaida kama alivyo sema Ibn Abbas r.a. Taz. Ibn Kathir) wala sitamwezesha mtu yeyote kukuuwa. Nami nitakunyanyua pahala pa utukufu wangu, na nitakuepusha na maadui wako wanao kusudia kukuuwa, na nitawafanya wanao kufuata wasio kengeuka na dini yako, wawe na nguvu na utawala juu ya wale wasio fuata uwongofu wako, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu ni Akhera. Hapo nitawahukumu katika hayo mlio kuwa mkizozana kwayo katika mambo ya dini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na vitimbi vya Allah Mtukufu kwao ni pale Aliposema Allah Mtukufu kumuambia ‛Ĩsã, Mimi nitakutwaa kutoka kwenye ardhi bila ya kupatikana na baya lolote, nitakuinua mpaka kwangu kwa mwili wako na roho yako, nitakuokoa na watu waliokukanusha na nitawafanya wale waliokufuata wewe, yaani,waliyo kwenye dini yako, na kufuata yale uliyokuja nayo kutoka kwa Allah Mtukufu ya dini na bishara ya Mtume Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, wakamuamini Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, baada ya kutumilizwa kwake, wakashikamana na Sheria aliyokuja nayo, wawe na ushindi juu ya wale walioukanusha utume wako hadi Siku ya Kiyama; kisha mwisho wenu nyote mtarudi kwangu Siku ya Hesabu, ili nitoe uamuzi juu ya tafauti mliokuwa nazo kuhusu ‛Ĩsã, amani imshukie.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net