Aal-i-Imraan 3:54
آل عمرانوَمَكَرُوا۟ وَمَكَرَ ٱللَّهُ ۖ وَٱللَّهُ خَيْرُ ٱلْمَـٰكِرِينَ
Na makafiri wakapanga vitimbi, na Mwenyezi Mungu akapanga vitimbi, na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wenye kupanga vitimbi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Makafiri walipanga mipango na Mwenyezi Mungu akapanga mipango, na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wenye kupanga. [54]
[54] Ama hao makafiri wapinzani walipanga njama za chini kwa chini kuupiga vita wito (Da'wa) wa Isa. Mwenyezi Mungu alizibat'ilisha njama zao, wasifanikiwe kuyapata waliyo yakusudia. Na Mwenyezi Mungu kwa hikima yake anawashinda watu wote wafanyao hila.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale waliomkanusha ‛Ĩsã, miongoni mwa Wana wa Isrãîl, walifanya vitimbi kwa kumpangia wenye kumuua. Allah Mtukufu akamtoa anayefanana na ‛Ĩsã kwa mtu ambaye aliwaashiria wauaji kwake, wakamshika wakamuua na wakamsulubu wakidhani kuwa ni ‛Ĩsã, amani imshukie. Na Allah Mtukufu ni bora wa wenye kufanya vitimbi. Katika haya pana kuthibitisha sifa ya makr (vitimbi) kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake na ukamilifu Wake, kwa kuwa ni vitimbi vya haki na ni katika kukabiliana na vitimbi vya wenye vitimbi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net