Aal-i-Imraan 3:53
آل عمرانرَبَّنَآ ءَامَنَّا بِمَآ أَنزَلْتَ وَٱتَّبَعْنَا ٱلرَّسُولَ فَٱكْتُبْنَا مَعَ ٱلشَّـٰهِدِينَ
Mola wetu Mlezi! Tuliyaamini uliyoyateremsha, na tulimfuata Mtume huyu, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mola wetu Mlezi! Tumeyaamini uliyo yateremsha, na tumemfuata huyu Mtume, basi tuandike pamoja na wanao shuhudia. [53]
[53] Na sisi tunasema: Ewe Mola Mlezi wetu! Tumekisadiki Kitabu chako ulicho mteremshia Nabii wako, na tunaifuata amri ya Mtume wako, Isa a.s. Basi tuthibitishe kuwa miongoni mwa wenye kumshuhudia Mtume wako katika kufikisha ujumbe, na kuwashuhudia Wana wa Israili katika ukafiri wao na upinzani wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Ewe Mola wetu! Tumeiamini Injili uliyoiteremsha na tumemfuata Mtume Wako ‛Ĩsã, amani imshukie, basi tujaalie ni miongoni mwa waliokutolea ushahidi juu ya umoja Wako na kuwatolea ushahidi Manabii juu ya utume wao.» Nao ni ummah wa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, ambao wanawatolea ushahidi mitume kuwa wao wamewafikishia ummah wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net