Aal-i-Imraan 3:52
آل عمرانفَلَمَّآ أَحَسَّ عِيسَىٰ مِنْهُمُ ٱلْكُفْرَ قَالَ مَنْ أَنصَارِىٓ إِلَى ٱللَّهِ ۖ قَالَ ٱلْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ ٱللَّهِ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَٱشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ
Isa alipohisi ukafiri miongoni mwao, akasema: Ni nani watakaonisaidia katika kulingania kwa Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wake wakasema: Sisi tutamnusuru Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Isa alipo hisi kuwa kati yao pana ukafiri alisema: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wake wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu. [52]
[52] Basi alipo kuja Isa a.s. akawaita watu wake wafuate Njia Iliyo Nyooka, wengi wao walikataa. Alipo yajua hayo aliwaelekea na kuwaambia: Ni nani atakaye nisaidia katika kazi hii niifanyayo ya kuitia kwenye Haki? Wakamjibu baadhi ya Waumini wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na yeye: Sisi tunakuunga mkono, na tutakusaidia, kwa sababu wewe ni Mwitaji, unaita watu wende kwa Mwenyezi Mungu. Na shuhudia kuwa sisi tumemsafia Mwenyezi Mungu na ni wenye kufuata amri zake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Alipohisi ‛Ĩsã kutoka kwao ukafiri, aliita kwa watu wake halisi kwa kusema, «Ni nani atakayekuwa na mimi katika kuinusuru dini ya Allah Mtukufu.» Wale wafuasi wa ‛Ĩsã walisema, «Sisi ni wenye kuinusuru dini ya Allah Mtukufu na wenye kuilingania, tumemuamini Allah Mtukufu na tumekufuata; na ushuhudie, ewe ‛Ĩsã, kuwa sisi tumejisalimisha kwa Allah Mtukufu kwa kumpwekesha na kumtii».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net