Aal-i-Imraan 3:70
آل عمرانيَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ
Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnazikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu ilhali nyinyi mnashuhudia?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi Watu wa Kitabu! Mbona mnazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu ilhali nyinyi mnashuhudia? [70]
[70] Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnakanusha Aya na Ishara za Mwenyezi Mungu zilizo teremka kuthibitisha Unabii wa Muhammad, s.a.w. na hali nyinyi mnaijua haki?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi watu wa Taurati na Injili! Vipi nyinyi mnakanusha aya za Allah Mtukufu ambazo aliziteremsha kwa Mitume wake katika Vitabu vyenu, na ndani yake muna kuwa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, ndiye Mtume anayengojewa na kuwa aliyowajia nayo ndio haki. Na nyinyi mnashuhudia hilo, lakini mnalikanusha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net