Aal-i-Imraan 3:71
آل عمرانيَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ لِمَ تَلْبِسُونَ ٱلْحَقَّ بِٱلْبَـٰطِلِ وَتَكْتُمُونَ ٱلْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ
Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnaivisha haki uongo, na mnaificha haki ilhali mnajua?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi Watu wa Kitabu! Mbona kweli mnaivisha uwongo, na kweli mnaificha na hali mnajua? [71]
[71] Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mkachukua Haki waliyo kuja nayo Manabii, na ikateremshiwa Vitabu, mkaichanganya na mambo ya udanganyifu ya kubuni na mkaleta tafsiri potovu, na msieneze Haki safi iliyo wazi isiyo kuwa na mchanganyiko? Na nyinyi mwajua vyema kuwa adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kitendo kama hichi ni kubwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi watu wa Taurati na Injili! Kwa nini nyinyi mnachanganya haki iliyo ndani ya vitabu vyenu, kwa yale ya ubatilifu mliyoyapotosha na kuyaweka kwa mikono yenu, na kuzificha kwenu sifa za Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, ziliomo ndani ya vitabu hivyo viwili na (kuficha kwenu) kwamba Dini yake ndiyo ya haki, na hali nyinyi mnajua hilo?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net