Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 72

Aal-i-Imraan 3:72

آل عمران

وَقَالَت طَّآئِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ ءَامِنُوا۟ بِٱلَّذِىٓ أُنزِلَ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَجْهَ ٱلنَّهَارِ وَٱكْفُرُوٓا۟ ءَاخِرَهُۥ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

Maana

Na kilisema kikundi kimoja katika Watu wa Kitabu: Yaaminini yale waliyoteremshiwa wale walioamini mwanzo wa mchana, na yakufuruni mwisho wake; huenda wakarejea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kikundi katika Watu wa Kitabu walisema: Yaaminini yale waliyo teremshiwa wenye kuamini mwanzo wa mchana, na yakataeni mwisho wake; huenda wakarejea. [72]

[72] Katika mtindo wao wa kutaka kuwapotoa Waumini, hawa Watu wa Kitabu wakiwaambia wenzao: Jitieni kuiamini Qur'ani aliyo teremshiwa Muhammad asubuhi, na ikifika jioni ikataeni. Huenda kwa hivyo mkawafitini hawa kwa kuwaingiza shaka katika nyoyo zao, wakaiacha dini yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na pote la watu wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi lilisema, Sadikini kilichoteremshwa kwa walioamini mwanzo wa mchana na mkanushe mwisho wake. Huenda wao wakafanya shaka juu ya dini yao na wakaiacha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net