Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 73

Aal-i-Imraan 3:73

آل عمران

وَلَا تُؤْمِنُوٓا۟ إِلَّا لِمَن تَبِعَ دِينَكُمْ قُلْ إِنَّ ٱلْهُدَىٰ هُدَى ٱللَّهِ أَن يُؤْتَىٰٓ أَحَدٌ مِّثْلَ مَآ أُوتِيتُمْ أَوْ يُحَآجُّوكُمْ عِندَ رَبِّكُمْ ۗ قُلْ إِنَّ ٱلْفَضْلَ بِيَدِ ٱللَّهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَآءُ ۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ

Maana

Wala msimuamini isipokuwa yule anayeifuata dini yenu. Sema: Hakika uongofu ni uongofu wa Mwenyezi Mungu, kuwa apewe mtu mfano wa yale mliyopewa nyinyi au wawahoji mbele ya Mola wenu Mlezi. Sema: Hakika fadhila zimo mkononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa hizo amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala msimuamini ila anaye fuata dini yenu. Sema: Hakika uwongofu ni uwongofu wa Mwenyezi Mungu, kuwa apewe mtu mfano wa mlio pewa nyinyi au wakuhojini mbele ya Mola wenu Mlezi. Sema: Hakika fadhila zimo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mjuzi. [73]

[73] Aidha wao husema: Msiwakubalie ila aliye fuata dini yenu, asije yeyote kati yao akadai kuwa nao wamepewa kama mlio pewa nyinyi, au akachukulia hoja mbele ya Mola wenu Mlezi kwa kuwakubalia kwenu. Ewe Nabii! Waambie: Hakika uwongofu wote unateremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye anaye mmiminia na kumteua amtakaye. Na ewe Nabii! Waambie: Hakika fadhila ziko kwa Mwenyezi Mungu humpa amtakaye katika waja wake, na Yeye ni Mkunjufu wa fadhila, Mjuzi wa anaye stahiki hayo na anaye teremkiwa na hayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

«Na msimsadiki kikweli isipokuwa yule aliyefuata dini yenu akawa Myahudi.» Waambie, ewe Mtume, «Uongofu na taufiki ni uongofu wa Allah Mtukufu na taufiki Yake ya kuongoza kwenye Imani sahihi.» Na walisema, «Msiidhihirishe kwa Waislamu elimu mlionayo, wasije wakajifunza kutoka kwenu wakawa sawa na nyinyi katika kuijua na wakawa na ubora juu yenu au wakaichukua kuwa ni hoja kutoka kwa Mola wenu wakawashinda kwayo.» Waambie, ewe Mtume, «Fadhila na vipawa na mambo yote yako mkononi mwa Allah Mtukufu na yako chini ya uendeshaji Wake, Anampa Amtakaye miongoni mwa waliomuamini Yeye na Mtume Wake. Allah Mtukufu ni Mkunjufu na ni Mjuzi: Anawaenea, kwa elimu Yake na upaji Wake, viumbe Vyake vyote vinavyostahiki fadhila Zake na neema Zake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net