Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 74

Aal-i-Imraan 3:74

آل عمران

يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِۦ مَن يَشَآءُ ۗ وَٱللَّهُ ذُو ٱلْفَضْلِ ٱلْعَظِيمِ

Maana

Yeye humchagua kumpa rehema zake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye humchagua kumpa rehema zake amtakaye; na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kubwa. [74]

[74] Yeye Mwenyezi Mungu humpa amtakaye Unabii na Utume, na anaye mkhusisha kwa kumpa hayo ni katika fadhila yake tu. Na Mwenyezi Mungu ana fadhila kubwa kubwa kabisa, na wala hapana anaye muingilia yeyote, wala hapana anaye mzuia katika kutoa kwake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Anawahusisha Anaowataka katika viumbe Wake kwa kuwapa utume na kuwaongoa kwenye Sheria kamilifu kabisa. Na Allah Mtukufu Ndiye Mwenye ihsani na upaji mwingi wenye kuenea.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net