Aal-i-Imraan 3:75
آل عمرانوَمِنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ مَنْ إِن تَأْمَنْهُ بِقِنطَارٍ يُؤَدِّهِۦٓ إِلَيْكَ وَمِنْهُم مَّنْ إِن تَأْمَنْهُ بِدِينَارٍ لَّا يُؤَدِّهِۦٓ إِلَيْكَ إِلَّا مَا دُمْتَ عَلَيْهِ قَآئِمًا ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا۟ لَيْسَ عَلَيْنَا فِى ٱلْأُمِّيِّـۧنَ سَبِيلٌ وَيَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ
Na miongoni mwa Watu wa Kitabu yupo ambaye ukimpa amana ya mrundo wa mali, atakurudishia. Na miongoni mwao yupo ambaye ukimpa amana ya dinari moja, hakurudishii isipokuwa ukimsimamia kumdai. Haya ni kwa kuwa walisema: 'Hatuna lawama kwa sababu ya hawa wasiojua kusoma na kuandika.' Na wanasema uongo juu ya Mwenyezi Mungu hali ya kuwa wanajua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na miongoni mwa Watu wa Kitabu yupo ambaye ukimpa amana ya mrundi wa mali atakurudishia, na miongoni mwao yupo ambaye ukimpa amana ya dinari moja hakurudishii isipo kuwa ukimsimamia kumdai. Haya ni kwa kuwa wakisema: Hatuna lawama kwa ajili ya hawa wasio jua kusoma. Na wanamzulia uwongo Mwenyezi Mungu, hali nao wanajua. [75]
[75] Huo ndio mwendo wao Watu wa Biblia katika itikadi, ama mwendo wao katika mambo ya mali utaona: Kati yao kuna ambaye ukimpa amana ya chungu ya dhahabu au fedha atakurejeshea sawa sawa bila ya kupunguka chochote. Na mwengine kati yao ukimpa amana ya dinari moja tu hakurudushii, ila ikiwa utamshikilia mpaka aitoe. Haya ni kwa sababu wapo baadhi yao wanawaona watu wa mataifa mengine, si watu wa Biblia basi haiwalazimu wao kuwatendea haki, na wanadai kuwa hiyo ni hukumu ya Mwenyezi Mungu. Na wao wanajua vyema kuwa hayo ni kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu. (Tazama katika Agano la Kale: Kumbukumbu la Torati, 23.19-20 inaruhusu kumnyonya riba mtu mbali asiyekuwa Yahudi. Kumbukumbu 12.21 inaruhusu kumlisha nyamafu mgeni na kumuuzia pia. Uzushi kama huu unakashifiwa na Aya 78 ifuatayo kuwa haya hayakutokana na Mwenyezi Mungu, bali wamepachika wao tu katika vitabu vyao.)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwa Watu wa Kitabu, katika Mayahudi, kuna ambaye lau utamuamini kwa mali mengi atakutekelezea bila hiana. Na miongoni mwao kuna ambaye lau utamuamini kwa dinari moja hatakutekelezea, mpaka ufanye juhudi kubwa ya kumfuata. Sababu ya hilo, ni itikadi mbovu inayowafanya wajihalalishie mali ya Waarabu kwa njia ya batili. Na wanasema, «Hatuna dhambi wala kosa kwa kula mali yao, kwa kuwa Allah Mtukufu ameyahalalisha kwetu.» Huu ni urongo wa kumzulia Allah Mtukufu; wanausema kwa ndimi zao na hali wanajua kuwa wao ni warongo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net