Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 76

Aal-i-Imraan 3:76

آل عمران

بَلَىٰ مَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِۦ وَٱتَّقَىٰ فَإِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُتَّقِينَ

Maana

Sivyo hivyo! Bali mwenye kulitimiza agano lake na akawa mcha Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wacha Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sivyo hivyo, bali anaye timiza ahadi yake na akamchamngu basi Mwenyezi Mungu huwapenda wachamngu. [76]

[76] Hakika ni kweli wamemzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Kwani mwenye kumrejeshea mwenyewe haki yake na akamtimizia kwa wakati wake kama alivyo ahidi, na akamwogopa Mwenyezi Mungu, wala asipunguze kitu wala asiakhirishe, huyo basi atapata mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa sababu amemcha Yeye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mambo si kama vile walivyodai hawa warongo. Mchaji Mungu kikweli ni yule aliyetekeleza ahadi aliyomuahidi Allah Mtukufu ya kutekeleza amana na kumuamini Yeye na Mitume Wake na akajilazimisha kufuata uongofu Wake na Sheria Yake na akamuogopa Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka, kwa kufuata Aliyoamrisha na kujiepusha na Aliyokataza. Na Allah Mtukufu Anawapenda wachamungu wenye kujikinga na ushirikina na maasia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net