Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 77

Aal-i-Imraan 3:77

آل عمران

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ ٱللَّهِ وَأَيْمَـٰنِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا أُو۟لَـٰٓئِكَ لَا خَلَـٰقَ لَهُمْ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ ٱللَّهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Maana

Hakika, wale wanaouza agano la Mwenyezi Mungu na viapo vyao kwa thamani ndogo, hao hawatakuwa na fungu lolote katika Akhera, wala Mwenyezi Mungu hatasema nao, wala hatawatazama Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, nao wana adhabu chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wanao uza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao thamani ndogo, hao hawatakuwa na sehemu ya kheri yoyote katika Akhera, wala Mwenyezi Mungu hatasema nao wala hatawatazama Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, nao watapata adhabu chungu. [77]

[77] Wanao iacha ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyo fungamana nao ya kuwa watazitimiza haki na watasimamia yaliyo waajibu, wala hawatoacha viapo vyao walivyo apa kuwa watatimiza - kwa thamani ndogo ya faida ya dunia, na ingawa kuu katika maoni yao, hao hawatakuwa na sehemu yoyote katika raha za Akhera. Mola wao Mlezi atawapuuza, wala hatowaangalia kwa jicho la rehema Siku ya Kiyama, wala hatowafutia dhambi zao, na watapata adhabu chungu ya kuendelea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale ambao wanabadilisha ahadi ya Allah Mtukufu na wasia Wake Aliowausia katika Vitabu Alivyowateremshia Mitume wao, kwa kupokea kitu kitwevu miongoni mwa vyombo vya ulimwengu na taka zake, wao hawana fungu la thawabu katika Akhera. Na Allah Mtukufu Hatasema na wao maneno ya kuwafurahisha; wala hatawaangalia kwa jicho la huruma Siku ya Kiyama na wala Hatawasafisha kutokana na uchafu wa madhambi na ukafiri. Na watakuwa na adhabu yenye kuumiza.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net