Aal-i-Imraan 3:78
آل عمرانوَإِنَّ مِنْهُمْ لَفَرِيقًا يَلْوُۥنَ أَلْسِنَتَهُم بِٱلْكِتَـٰبِ لِتَحْسَبُوهُ مِنَ ٱلْكِتَـٰبِ وَمَا هُوَ مِنَ ٱلْكِتَـٰبِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنْ عِندِ ٱللَّهِ وَمَا هُوَ مِنْ عِندِ ٱللَّهِ وَيَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ
Na hakika wapo miongoni mwao kundi lipindualo ndimi zao katika kusoma Kitabu ili mdhani kuwa hayo yanatoka Kitabuni, na wala hayatoki Kitabuni. Nao husema: 'Haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu.' Na wala hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na wanasema uongo juu ya Mwenyezi Mungu hali ya kuwa wanajua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wapo baadhi yao wanao pindua ndimi zao katika kusoma Kitabu ili mdhanie kuwa hayo yanatoka Kitabuni, na wala hayatoki Kitabuni. Na husema: Haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu. Na wala hayatoki kwa Mwenyezi Mungu. Na wanamsingizia Mwenyezi Mungu uwongo na wao wanajua. [78]
[78] Katika Watu wa Kitabu wapo ambao huzipindua ndimi zao kutamka maneno yasiyo kuwamo katika Kitabu kwa lafdhi ya Kitabu, watu wadhanie kuwa ni maneno yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu, na wala hayamo katika ufunuo wa Mwenyezi Mungu. Wanamzulia Mwenyezi Mungu nao ndani ya nafsi zao wanajua kuwa wanasema uwongo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Miongoni mwa Mayahudi kuna watu wanaoyapotoa maneno na kuyaondoa mahali pake. Na wanayabadilisha maneno ya Allah Mtukufu, ili kuwafanya wasiokuwa wao wadhanie kuwa hayo ni miongoni mwa maneno yaliyoteremshwa katika Taurati, nayo si katika maneno yaliyomo kwenye Taurati kabisa, na wanasema, «Haya yanatoka kwa Allah Mtukufu, yameletwa kwa Nabii Wake Mûsã kwa njia ya wahyi.» Nayo hayatoki kwa Allah Mtukufu. Na wao, kwa ajili ya ulimwengu wao, wanasema urongo kumzulia Allah Mtukufu, na hali wanajua kuwa wao ni warongo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net