Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 79

Aal-i-Imraan 3:79

آل عمران

مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤْتِيَهُ ٱللَّهُ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحُكْمَ وَٱلنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُوا۟ عِبَادًا لِّى مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَـٰكِن كُونُوا۟ رَبَّـٰنِيِّـۧنَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ ٱلْكِتَـٰبَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ

Maana

Haikumfailia mtu yeyote kwamba Mwenyezi Mungu ampe Kitabu na hekima na Unabii, kisha awaambie watu: 'Kuweni wa kuniabudu mimi badala ya Mwenyezi Mungu.' Bali atawaambia: 'Kuweni wenye kumuabudu Mola Mlezi wa viumbe vyote, kwa kuwa nyinyi mnafundisha Kitabu na kwa kuwa mnakisoma.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Haiwezi kuwa mtu aliye pewa na Mwenyezi Mungu Kitabu na hikima na Unabii kisha awaambie watu: Kuweni wa kuniabudu mimi badala ya Mwenyezi Mungu. Bali atawaambia: Kuweni wenye kumuabudu Mola Mlezi wa viumbe vyote, kwa kuwa nyinyi mnafundisha Kitabu na kwa kuwa mnakisoma. [79]

[79] Si akili wala haimfalii mwanaadamu aliye teremshiwa Kitabu na Mwenyezi Mungu na akapewa ilimu ya manufaa na kuweza kuzungumza mambo yanayo tokana na Mwenyezi Mungu, tena awatake watu wamuabudu yeye badala ya kumuabudu Mwenyezi Mungu. Lakini linalo ingia akilini, na lifaalo, ni kuwa yeye awatake watu wamsafie ibada Mola wao Mlezi aliye waumba kwa mujibu alivyo wafunza kutokana na ilimu ya Kitabu na kwa mujibu ya wanayo soma.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Haitakiwi kwa binadamu yoyote ateremshiwe kitabu na Allah Mtukufu chenye kutoa uamuzi kwa viumbe Wake na achaguliwe kuwa ni Nabii, kisha awaambie watu, «Niabuduni mimi badala ya Allah Mtukufu.» Lakini atasema, «Kuweni ni watu wa busara, wenye kuelewa na wajuzi wa wahyi wa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, mliokuwa mkiwafundisha wengine na mnaousoma kwa kuuhifadhi, kuujua na kuuelewa».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net