Aal-i-Imraan 3:80
آل عمرانوَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا۟ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ أَرْبَابًا ۗ أَيَأْمُرُكُم بِٱلْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ
Wala hatawaamrisha kwamba muwafanye Malaika na Manabii kuwa ni miungu. Je, atawaamrisha ukafiri baada ya nyinyi kuwa Waislamu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala hatakuamrisheni kuwafanya Malaika na Manabii kuwa ni miungu. Je, atakuamrisheni ukafiri baada ya kuwa nyinyi Waislamu? [80]
[80] Wala hayumkini akuamrisheni kuwafanya Malaika au Manabii kuwa ndio miungu badala ya Mwenyezi Mungu. Ni ukafiri usio ingia akilini kukuamrisheni hayo baada ya kuwa mmekwisha kuwa Waislamu mlio muelekezea nyuso Mwenyezi Mungu. (Nabii Isa a.s. hakujidaia Ungu hata katika Injili hizi zilizo korogwa, wala hakumfanya Roho Mtakatifu, ambaye ni Malaika, kuwa ni Mungu.)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na haikuwa kwa yoyote katika wao awaamrishe nyinyi kuwafanya Malaika na Mitume ni waungu wasiokuwa Allah Mtukufu ambao nyinyi mnawaabudu. Je, inaingia akilini, enyi watu, yeye awaamrishe kumkanusha Allah Mtukufu baada ya kufuata kwenu amri yake?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net