Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 81

Aal-i-Imraan 3:81

آل عمران

وَإِذْ أَخَذَ ٱللَّهُ مِيثَـٰقَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ لَمَآ ءَاتَيْتُكُم مِّن كِتَـٰبٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَآءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِۦ وَلَتَنصُرُنَّهُۥ ۚ قَالَ ءَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِى ۖ قَالُوٓا۟ أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَٱشْهَدُوا۟ وَأَنَا۠ مَعَكُم مِّنَ ٱلشَّـٰهِدِينَ

Maana

Na pale Mwenyezi Mungu alipochukua agano la Manabii: Nikishawapa Kitabu na hekima, kisha akawajia Mtume mwenye kusadikisha yale mliyo nayo, basi hakika mtamuamini na mtamsaidia. Akasema: Je, mmekiri na mmekubali kushika agano langu la mkazo juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni, na Mimi ni pamoja nanyi katika wanaoshuhudia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pale Mwenyezi Mungu alipo chukua ahadi kwa Manabii: Nikisha kupeni Kitabu na hikima, kisha akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo, ni juu yenu mumuamini na mumsaidie. Akasema: Je, mmekiri na mmekubali kushika agizo langu juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni, na Mimi ni pamoja nanyi katika kushuhudia. [81]

[81] Ewe Nabii! Watajie kuwa Mwenyezi Mungu aliahidiana na akaagana na kila Nabii aliye teremshiwa Kitabu na akapewa ilimu ya manufaa, ya kwamba akija Mtume ambaye wito wake unakubaliana na wito wao basi ni waajibu wao wamuamini na wamsaidie. Na Manabii wote walikiri kuitimiza ahadi hiyo, na wakakiri na wakashuhudia kwa nafsi zao, na Mwenyezi Mungu akawashuhudia hayo. Tena wao wakayafikisha hayo kwa kaumu zao. Ahadi hiyo imewapasia wao imani na wamnusuru wakimwahi. Kama hawakumwahi basi ni waajibu wa kaumu zao wamuamini na wamnusuru kwa kutimiza na kufuata yaliyo walazimu Manabii wao.(Tazama katika Biblia: Kumbukumbu 18.17-19, Injili ya Yohana 16.7-14)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kumbuka, ewe Mtume, pindi Alipochukua Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ahadi ya mkazo kwa Manabii wote kwamba, «Nikiwaletea Kitabu na hekima kisha akaja kwenu mjumbe kutoka kwangu, mwenye kusadikisha vitabu mlivyonavyo, mtamuamini na kumnusuru? Je, mumekiri na kukubali hilo na mumechukua juu yake ahadi yangu ya mkazo?» Wakasema, «Tumekubali hilo.» Akasema, «Kueni mashahidi, baadhi yenu juu ya wengine, na kueni mashahidi kwa hilo juu ya ummah wenu, na mimi ni Mwenye kushuhudia pamoja na nyinyi juu yenu na juu yao». Katika haya pana ahadi nzito Aliyoichukua Allah Mtukufu kutoka kwa kila Nabii amuamini Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na kuchukua ahadi nzito kutoka kwa ummah wa Manabii wote juu ya hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net