Aal-i-Imraan 3:82
آل عمرانفَمَن تَوَلَّىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَـٰسِقُونَ
Kwa hivyo, mwenye kugeuka baada ya haya, basi hao ndio wavukao mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Watakao geuka baada ya haya basi hao ndio wapotovu. [82]
[82] Anaye kataa kumuamini Nabii huyu baada ya ahadi hii madhubuti ni mpotovu aliye toka kwenye sharia ya Mwenyezi Mungu, ni kafiri mwenye kuwakataa Manabii wote wa mwanzo mpaka wa mwisho.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi mwenye kuupa mgongo ulinganizi wa Uislamu baada ya maelezo haya na ahadi hii Aliyoichukuwa Allah Mtukufu kutoka kwa Manabii Wake, hao ndio wenye kutoka nje ya dini ya Allah Mtukufu na twaa ya Mola wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net