Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 83

Aal-i-Imraan 3:83

آل عمران

أَفَغَيْرَ دِينِ ٱللَّهِ يَبْغُونَ وَلَهُۥٓ أَسْلَمَ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ

Maana

Je, wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu, ilhali kila kilicho katika mbingu na katika ardhi kimejisalimisha kwake kwa kumtii Yeye kwa kupenda na kwa kutopenda, na kwake Yeye watarejeshwa?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu kwa kumt'ii Yeye kikipenda kisipende, na kwake Yeye watarejeshwa? [83]

[83] Je, wanataka Dini isiyo kuwa Dini ya Muhammad, na hiyo ndiyo Dini ya Manabii wote? Dini hii ndiyo pekee Dini ya Mwenyezi Mungu anaye nyenyekewa na kila kilichomo mbinguni na duniani kwa ut'iifu, kwa kupenda na khiari, au kwa lazima kwa kufuata tabia na maumbile. Na kwake Yeye ndio viumbe vyote vinarejea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, wanataka hawa wenye kutoka nje ya twaa ya Allah Mtukufu, miongoni mwa Watu wa Kitabu, dini isiyokuwa dini ya Allah Mtukufu nayo ni Uislamu ambao Allah Mtukufu Alimtumiliza nao Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, hali ya kuwa wote walioko mbinguni na ardhini wamejisalimisha na kufuata na kunyenyekea kwa Allah Mtukufu kwa hiyari, kama walivyo Waumini, na kwa kulazimika wakati wa shida ambapo hilo haliwanufaishi, nao ni makafiri, kama vilivyonyenyekea Kwake viumbe vyote. Na Kwake watarejeshwa Siku ya Marejeo, na alipwe kila mmoja kwa amali yake? Hili ni onyo kutoka kwa Allah Mtukufu kwa yoyote, katika viumbe Vyake, atakayerudi Kwake juu ya mila isiyokuwa ya Kiislamu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net