Aal-i-Imraan 3:84
آل عمرانقُلْ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ عَلَيْنَا وَمَآ أُنزِلَ عَلَىٰٓ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْمَـٰعِيلَ وَإِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ وَٱلْأَسْبَاطِ وَمَآ أُوتِىَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَٱلنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُۥ مُسْلِمُونَ
Sema: Tumemwamini Mwenyezi Mungu, na yale tuliyoteremshiwa sisi, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na Yaakub na wana wake, na yale aliyopewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi. Hatutofautishi yeyote baina yao, na sisi ni wenye kujisalimisha kwake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyo teremshiwa sisi, na aliyo teremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na Yaakub na wajukuu zao, na aliyo pewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi. Hatubagui baina yao hata mmoja, na sisi ni wenye kusilimu kwake. [84]
[84] Mwenyezi Mungu ametilia mkazo kuwa Yeye ni Mmoja, na Ujumbe wake ni mmoja. Amemuamrisha Nabii wake na walio pamoja naye wasema: Tumesadiki kuwa Mwenyezi Mungu ndiye peke yake anaye faa kuabudiwa, na ndiye anaye watuma Mitume wake. Na tumeiamini Qur'ani na Sharia aliyo tuteremshia Mwenyezi Mungu, na pia tumeamini Vitabu na Sharia alizo wateremshia Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na watoto wao thinaashara, na aliyo teremsha Mwenyezi Mungu kwa Musa, nayo ni Taurati, na kwa Isa, nayo ni Injili, na walio teremshiwa Manabii wote walio baki. Hapana khitilafu katika kuamini baina ya yeyote katika wao. Na sisi kwa hivyo tumeuelekeza uso wetu kwa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waambie, ewe Mtume, Tumemuamini Allah Mtukufu na tumetii. Hatuna Mola isipokuwa Yeye, na hatuna muabudiwa isipokuwa Yeye. Tumeuamini wahyi Aliouteremsha kwetu na ule Aliouteremsha kwa Ibrãhîm aliye rafiki halisi wa Allah Mtukufu, na wanawe wawili, Ismã‘îl na Isḥãq, na mwana wa mwanawe,Ya‛qûb mwana wa Is’ḥāq, na Asbãṭ: nao ni Manabii waliokuwa katika makabila kumi na mbili wanaotokana na watoto wa Ya‛qûb, na wahyi uliopewa Mûsã na ‘Ǐsâ wa Taurati na Injili, na wahyi Aliouteremsha Allah Mtukufu kwa Manabii Wake. Tunayaamini hayo yote. Wala hatumbagui yoyote katika wao. Na sisi tunamfuata Allah Mtukufu Peke Yake kwa kumtii na kumuabudu, tunakiri Kwake kuwa Yeye Ndiye Mola, Ndiye Mungu na Ndiye wa kuabudiwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net