Aal-i-Imraan 3:200
آل عمرانيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱصْبِرُوا۟ وَصَابِرُوا۟ وَرَابِطُوا۟ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
Enyi mlioamini! Subirini, na vumilieni, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufaulu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa. [200]
[200] Enyi mlio amini! Shikamaneni na subira, na mwashinde maadui zenu katika kusubiri. Na kaeni macho kuilinda mipaka, na mkhofini Mola Mlezi wenu. Katika haya yote ndio mtaraji kufanikiwa. (Jee! Baada ya kuijua Qur'ani yamfalia Muislamu kusema kuwa dini ni kitu mbali na siyasa? Vipi uamrishe mema, ukataze maovu, uhukumu, ukatibiane mikataba na dola nyengine, ukusanye zaka na kuzigawa, upigane Jihadi, ulinde mipaka n.k., n.k. na uiepuke siyasa? Amesema Prof. Khurshid Ahmad: "Uislamu si dini kwa maana ya ovyo ovyo kama lilivyo potoshwa neno hilo, yaani kuwa umemkhusu mtu maisha yake ya binafsi tu. Ni mwendo kaamili wa maisha, unao angalia kila midani ya uhai wa binaadamu. Uislamu ni uwongozi katika kila nyendo za maisha - za binafsi na za jamii, za kimwili na kiroho, za uchumi na siyasa, za sharia na mila, za taifa na za mataifa."--Uislamu, Maana na Ujumbe wake uk. 37)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, kuweni na subira juu ya kumtii Mola wenu na juu yaliyowashukia ya madhara na shida, na washindeni maadui zenu katika kusubiri wasipate kuwa wasubirifu zaidi kuliko nyinyi, na simameni wima katika kumpiga vita adui yangu na adui yenu. Na muogopeni Allah Mtukufu, katika hali zenu zote, ili mfaulu kupata radhi Zake ulimwenguni na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net