Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 1

An-Nisaa 4:1

النساء

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُوا۟ رَبَّكُمُ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَٰحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَآءً ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ٱلَّذِى تَسَآءَلُونَ بِهِۦ وَٱلْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا

Maana

Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi ambaye aliwaumba kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka kwayo. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume wengi na wanawake. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaomba, na jamaa zenu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni. [1]

[1] Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na kutokana na nafsi hiyo akamuumba mkewe, na kutokana na hao wawili, wakaenea wanaume na wanawake wengi. Basi nyote mnatokana na nafsi moja. Mcheni Mwenyezi Mungu mnaye mtaka msaada kwa kila mnacho kihitajia, na kwa jina lake ndio mnaombana nyinyi kwa nyinyi katika mambo yenu. Pia tahadharini na kuacha kuwasaidia jamaa zenu, wa karibu na wa mbali. Kwani Mwenyezi Mungu daima anakuangalieni. Hapana chochote katika mambo yenu kinacho fichikana kwake. Na Yeye ndiye Mwenye kukulipeni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu, muogopeni Allah Mtukufu, mjilazimishe na amri Zake na mjiepushe na makatazo Yake. Kwani Yeye Ndiye Aliyewaumba nyinyi kutokana na nafsi moja, nayo ni Ãdam, amani imshukiye, na Akaiuumba, kutokana na nafsi hiyo, ya pili yake, nayo ni Ḥawwã. Na Akaeneza, kutokana na nafsi mbili hizo, wanaume wengi na wanawake wengi katika sehemu za ardhi hii. Na muogopeni Allah Mtukufu Ambaye kupitia Kwake mnaombana nyinyi kwa nyinyi. Na jihadharini msije mkakata udugu. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye kuzifuatilia hali zenu zote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net