An-Nisaa 4:2
النساءوَءَاتُوا۟ ٱلْيَتَـٰمَىٰٓ أَمْوَٰلَهُمْ ۖ وَلَا تَتَبَدَّلُوا۟ ٱلْخَبِيثَ بِٱلطَّيِّبِ ۖ وَلَا تَأْكُلُوٓا۟ أَمْوَٰلَهُمْ إِلَىٰٓ أَمْوَٰلِكُمْ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ حُوبًا كَبِيرًا
Na wapeni mayatima mali zao. Wala msibadilishe kibaya kwa kizuri. Wala msile mali zao pamoja na mali zenu. Hakika, yote hayo ni dhambi kubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wapeni mayatima mali yao. Wala msibadilishe kibaya kwa kizuri. Wala msile mali zao pamoja na mali zenu. Hakika yote hayo ni jukumu kubwa. [2]
[2] Na wapeni mayatima mali yao wanayo stahiki, na yalindeni mali yao vizuri, wala msiwape kilio duni mkawanyima kizuri. Wala msichukue mali yao mkaongezea kwenye mali yenu. Hakika kitendo hicho ni dhambi kubwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale waliofiliwa na baba zao wakiwa bado hawajabaleghe, na mkawa nyinyi ndio wasimamizi wao, wapeni mali zao wafikapo umri wa kubaleghe, muonapo kutoka kwao kuwa wana uwezo wa kuhifadhi mali zao. Na wala msichukuwe kizuri katika mali zao na mkaweka mahali pake kibaya katika mali zenu. Wala msichanganye mali zao na mali zenu ili mpate kula mali zao kwa hila. Na mwenye kujasiri kulitenda hilo, hakika huyo amefanya dhambi kubwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net