Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 199

Aal-i-Imraan 3:199

آل عمران

وَإِنَّ مِنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ لَمَن يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْهِمْ خَـٰشِعِينَ لِلَّهِ لَا يَشْتَرُونَ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۗ أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلْحِسَابِ

Maana

Na hakika, miongoni mwa Watu wa Kitabu kuna wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu na yaliyoteremshwa kwenu na yaliyoteremshwa kwao, wakimnyenyekea Mwenyezi Mungu. Hawanunui kwa Aya za Mwenyezi Mungu thamani ndogo. Hao wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu.[1]

[1] Imani yao ilipokuwa ya ujumla (bila ya kutofautisha baina ya Manabii na Vitabu), na ya uhakika, ikawa ni ya manufaa. Kwa hivyo, ikawafanya kumnyenyekea Mwenyezi Mungu. Na katika ukamilifu wa kumnyenyekea kwao Mwenyezi Mungu ni kwamba, "hawanunui kwa Aya za Mwenyezi Mungu thamani ndogo." Kwa hivyo, hawaitangulizi dunia mbele ya dini kama walivyofanya watu wa upotovu, ambao wanaficha yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na kununua kwayo thamani ndogo. Na wakajua kwamba katika hasara kubwa zaidi ni kutosheka na kilicho duni badala ya dini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika miongoni mwa Watu wa Kitabu wapo wanao muamini Mwenyezi Mungu na yaliyo teremshwa kwenu na yaliyo teremshwa kwao, wakimnyenyekea Mwenyezi Mungu. Hawabadili Aya za Mwenyezi Mungu kwa thamani duni. Hao wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu. [199]

[199] Hakika baadhi ya Watu wa Kitabu, Mayahudi na Wakristo, wanamuamini Mwenyezi Mungu, na wanaamini aliyo teremshiwa Nabii Muhammad s.a.w. na walio teremshiwa Mitume walio kuwa kabla yake. Utawaona wanamnyenyekea Mwenyezi Mungu, na wanakuwa wanyonge kwake, wala hawabadilishi bayana zilizo dhaahiri kwa ajili ya kutafuta pato la duniani. Hilo nalingawa kubwa ni kitu duni. Hawa wana malipo ya ukamilifu kwa Mola wao Mlezi katika makaazi ya kuridhisha. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu, hashindwi kuzidhibiti 'amali zao zote na kuwahisabia. Yeye ni Muweza wa hayo na malipo yake yatawafika bila ya shaka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Baadhi ya waliopewa vitabu wanamuamini Allah Mtukufu kuwa ni Mola Mmoja na Mungu Mwenye kuabudiwa, wanaiamini Qur’ani mliyoteremshiwa nyinyi na Taurati na Injili walizoteremshiwa wao, hali ya kumdhalilikia Allah Mtukufu na kumnyenyekea. Hawazibadilishi aya za Allah Mtukufu kwa thamani ndogo ya takataka za duniani wala hawayafichi Aliyoyataremsha Allah Mtukufu na wala hawayapotoshi kama wanavyofanya wengineo miongoni mwa waliopewa Vitabu. Hao watapata thawabu kubwa mbele ya Mola wao Siku ya kukutana Naye, na watapewa malipo yao kamili, bila ya kupunguzwa. Hakika Allah Mtukufu ni Mwepesi wa kuhesabu. Hakumshindi Yeye kuyadhibiti matendo yao na kuwahesabu wao kwayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net