Aal-i-Imraan 3:198
آل عمرانلَـٰكِنِ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ رَبَّهُمْ لَهُمْ جَنَّـٰتٌ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَا نُزُلًا مِّنْ عِندِ ٱللَّهِ ۗ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ خَيْرٌ لِّلْأَبْرَارِ
Lakini wale waliomcha Mola wao Mlezi wana Mabustani yanayopita mito chini yake. Watadumu humo. Hayo ni makaribisho yao yatokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na vilivyo kwa Mwenyezi Mungu ni bora kwa walio wema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lakini walio mcha Mola wao Mlezi watapata Mabustani yanayo pita mito kati yake. Watadumu humo. Hayo ni makaribisho yao yatokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na vilioko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kwa watu wema. [198]
[198] Hayo ndiyo malipo ya makafiri. Ama walio muamini Mwenyezi Mungu wakamwogopa Mola wao Mlezi watapata Mabustani yapitayo mito kati yake, watadumu humo daima, kuwa ni wageni walio pokewa kwa ukarimu na Mwenyezi Mungu, Subhanahu, Aliye takasika. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ndio mazuri kwa watu wema kuliko hayo wanayo starehea makafiri ambayo yataondoka, hayadumu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Lakini wale waliomuogopa Mola wao, wakazifuata amri Zake na wakajiepusha na makatazo Yake, Allah Mtukufu Amewaandalia mabustani ya Pepo ambayo mito inapita chini ya majumba yake ya fahari na miti yake. Mabustani hayo yatakuwa ni makazi yao ya kudumu; hawatatoka humo. Na yaliyoko kwa Allah Mtukufu ni makubwa zaidi na bora zaidi kwa watiifu kuliko yale ya starehe za ulimwengu ambazo hao waliokufuru wanatanga huku na kule kwa kuzitafuta.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net