Aal-i-Imraan 3:197
آل عمرانمَتَـٰعٌ قَلِيلٌ ثُمَّ مَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ ۚ وَبِئْسَ ٱلْمِهَادُ
Hiyo ni starehe ndogo. Kisha makazi yao yatakuwa Jahannamu. Na ni pahali pabaya mno pa kupumzikia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hiyo ni starehe ndogo. Kisha makaazi yao yatakuwa Jahannamu. Na ni mahali pabaya mno pa kupumzikia. [197]
[197] Hizo ni starehe za kupita njia, na kila kipitacho ni duni. Kisha marejeo ya daima watayo ishia ni Jahannamu. Na hapana makaazi maovu kama Jahannamu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hiyo ni starehe ndogo yenye kuondoka.Kisha marejeo yao Siku ya Kiyama ni Motoni. Na huo Moto ni tandiko ovu mno.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net