Aal-i-Imraan 3:196
آل عمرانلَا يَغُرَّنَّكَ تَقَلُّبُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِى ٱلْبِلَـٰدِ
Kamwe kusiwadanganye kutangatanga kwa wale waliokufuru katika nchi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kabisa kusikudanganye kubakia kutangatanga kwa walio kufuru katika nchi. [196]
[196] Usiathirike, ewe Nabii, kwa kuwaona makafiri wamo katika starehe za neema, na biashara na uchumi unawaendea, wakienda huku na huku katika nchi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Usihadaike, ewe Mtume, kwa yale waliyonayo wenye kumkufuru Allah Mtukufu, ya ukunjufu wa riziki, hali nzuri ya maisha na kuhama kwao kutoka mahali kwenda pengine kwa ajili ya biashara na kutaka faida na mali. Kwa muda mchache, yote hayo yatawaondokea na watakuwa ni wenye kufungika na kuwekwa dhamana kwa vitendo vyao viovu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net