Aal-i-Imraan 3:183
آل عمرانٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ عَهِدَ إِلَيْنَآ أَلَّا نُؤْمِنَ لِرَسُولٍ حَتَّىٰ يَأْتِيَنَا بِقُرْبَانٍ تَأْكُلُهُ ٱلنَّارُ ۗ قُلْ قَدْ جَآءَكُمْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِى بِٱلْبَيِّنَـٰتِ وَبِٱلَّذِى قُلْتُمْ فَلِمَ قَتَلْتُمُوهُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
Waliosema: Hakika, Mwenyezi Mungu alituusia kwamba tusimwamini Mtume yeyote mpaka atujie na kafara inayoliwa na moto. Waambie: Walikujieni Mitume kabla yangu kwa hoja zilizo wazi na kwa hayo mnayosema. Basi kwa nini mliwaua ikiwa nyinyi ni wakweli?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Walio sema: Mwenyezi Mungu ametuahidi tusimuamini Mtume yeyote mpaka atuletee kafara inayo teketezwa na moto. Waambie: Walikujieni Mitume kabla yangu kwa hoja zilizo wazi na kwa hayo mnayo sema, basi kwa nini mkawauwa ikiwa mlikuwa wakweli?. [183]
[183] Hao ndio walio sema: Mwenyezi Mungu ametuamrisha katika Taurati tusimfuate Mtume yeyote ila akileta dalili ya ukweli wake kwa kutuletea kitu cha kumkurubisha kwenye radhi ya Mwenyezi Mungu, na uteremke moto kutoka mbinguni ukile hicho kitu. Ewe Nabii! Waambie: Hakika Mitume kutoka kwa Mwenyezi Mungu wamekwisha kukujieni kabla yangu, wakaja na dalili zilizo wazi, na wakaja na hayo mnayo yasema. Na juu ya hayo mliwakadhibisha na mkawauwa. Kwa nini mkafanya hayo kama nyinyi ni wasema kweli katika ahadi yenu ya Imani yanapo timia mnayo yataka?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mayahudi hawa walipoitwa kuufuata Uislamu, walisema, «Allah Mtukufu Ametuusia katika Taurati kwamba tusimsadiki yoyote atakayetujia na neno la kwamba yeye ni mjumbe kutoka kwa Allah Mtukufu mpaka atuletee sadaka, ambayo kwayo atajisogeza karibu na Allah Mtukufu, hapo ushuke moto kutoka mbinguni uiteketeze.» Sema uwaambie,ewe Mtume, «Nyinyi ni warongo kwa hayo mnayoyasema. Kwani mababa zenu kabla yangu walijiliwa na Mitume, wakiwa na hoja na dalili za ukweli wao na pia hayo mliyoyasema ya kuleta sadaka ambayo itateketezwa na moto. Basi mbona mababa zenu waliwaua Mitume hao, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net