Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 182

Aal-i-Imraan 3:182

آل عمران

ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيكُمْ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَيْسَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ

Maana

Hayo ni kwa sababu ya iliyotanguliza mikono yenu, na kwamba Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Haya ni kwa sababu ya iliyo tanguliza mikono yenu, na kwamba Mwenyezi Mungu si mwenye mu waja. [182]

[182] Na hiyo adhabu ni kwa dhambi zao walizo zitenda wenyewe, na malipo ya Mwenyezi Mungu hayawi ila ni kwa uadilifu, wala Yeye kabisa hawadhulumu waja wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Adhabu hiyo kali ni kwa sababu ya yale mliyoyatanguliza katika maisha yenu ya duniani kati ya maasia ya kimaneno, ya kivitendo na ya kiitikadi, na kwamba Allah Mtukufu si Mwenye kuwadhulumu waja Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net