Aal-i-Imraan 3:181
آل عمرانلَّقَدْ سَمِعَ ٱللَّهُ قَوْلَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَآءُ ۘ سَنَكْتُبُ مَا قَالُوا۟ وَقَتْلَهُمُ ٱلْأَنۢبِيَآءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَنَقُولُ ذُوقُوا۟ عَذَابَ ٱلْحَرِيقِ
Hakika Mwenyezi Mungu amekwishasikia kauli ya wale waliosema: 'Hakika, Mwenyezi Mungu ni fakiri, na sisi ni matajiri.' Tutayaandika yale waliyoyasema, na pia kuwaua kwao Manabii bila ya haki, na tutawaambia Siku ya Kiyama: Onjeni adhabu ya kuunguza.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu amekwisha sikia kauli ya walio sema: Mwenyezi Mungu ni masikini, na sisi ni matajiri. Tumeyaandika waliyo yasema, na pia kuwauwa kwao Manabii bila ya haki, na tutawaambia Siku ya Kiyama: Onjeni adhabu ya kuungua. [181]
[181] Juu ya kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kumiliki kila kiliomo mbinguni na ardhini na Yeye ndiye mrithi wa vyote, wamesema baadhi ya Mayahudi kwa kejeli: Mwenyezi Mungu ni fakiri, ndiyo akatutaka tutoe, na sisi ni matajiri tukitoa au tusitoe. Mwenyezi Mungu amekwisha isikia kauli yao hiyo, na ameisajili dhidi yao, kama alivyo sajili kuwauwa kwao Manabii kwa dhulma na ukhalifu na uadui. Naye atawaambia Siku ya Kiyama: Onjeni adhabu ya Moto unao waka!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Amelisikia Allah Mtukufu neno la Mayahudi ambao walisema, «Allah Mtukufu ni muhitaji kwetu, Anatutaka tumkopeshe mali, na sisi ni matajiri.» Tutaliandika neno hili walilolisema na tutaandika kwamba wao wako radhi na yale yaliyofanyika ya kwamba mababa zao waliwaua Manabii wa Allah Mtukufu kwa dhuluma na uadui. Tutawaadhibu kwa hilo huko Akhera na tutawaambia, nao wamo Motoni waadhibiwa, «Ionjeni adhabu ya Moto unaounguza».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net