Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 180

Aal-i-Imraan 3:180

آل عمران

وَلَا يَحْسَبَنَّ ٱلَّذِينَ يَبْخَلُونَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ هُوَ خَيْرًا لَّهُم ۖ بَلْ هُوَ شَرٌّ لَّهُمْ ۖ سَيُطَوَّقُونَ مَا بَخِلُوا۟ بِهِۦ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ وَلِلَّهِ مِيرَٰثُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ

Maana

Wala wasidhani kabisa wale ambao wanafanya ubahili katika aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake kuwa ni heri kwao. Bali hiyo ni shari kwao. Watafungwa shingoni yale waliyoyafanyia ubahili Siku ya Kiyama. Na urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ana habari za yote myatendayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala wasidhani wale ambao wanafanya ubakhili katika aliyo wapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake kuwa ni kheri yao. Bali hiyo ni shari kwao. Watafungwa kongwa za yale waliyo yafanyia ubakhili Siku ya Kiyama. Na urithi wa Mbingu na Ardhi ni wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote myatendayo. [180]

[180] Wasidhani wanao fanya ubakhili kwa mali aliyo waneemesha Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na hawayatoi katika yaliyo waajibu na njia za kheri, kuwa ubakhili huo ni kheri yao. Bali hiyo ni shari yenye matokeo mabaya juu yao. Watalipwa malipo maovu kabisa Siku ya Kiyama, na adhabu itawaganda kama kongwa au mnyororo aliyo fungwa nayo mfungwa shingoni mwake. Kila kiumbe kinamnyenyekea Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la, naye ndiye Mmiliki wao, na Yeye Aliye takasika anajua kila mnacho kitenda, na atakulipeni kwacho.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wala wasidhani wale wanaozifanyia ubakhili neema za Allah Mtukufu Alizowaneemesha kwa kuwafadhili kwamba ubakhili huo ni bora kwao. Bali hiyo ni shari kwao. Kwani mali hayo waliyoyakusanya yatakuwa ni kitanzi cha moto kitakachowekwa shingoni mwao Siku ya Kiyama. Na Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Ndiye Mwenye kumiliki ufalme ; na Yeye Ndiye Atakayesalia baada ya kutoweka viumbe Wake wote. Yeye Ndiye Mtambuzi wa matendo yenu yote, na Atamlipa kila mtu kwa kadiri anayostahiki.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net